SAFARI YA KUELEKEA NYUMBA YA AKHERA


                                                           بسم الله الرحمن الرحيم.
                                                              الرحلة الى دار الآخرة
                                          SAFARI YA KUELEKEA NYUMBA YA AKHERA

IMEANDIKWA NA :ABDULBARRY
         Phone no: +255 778 682 699        
+249 992 261 471        
Email: suleimans003@gmail.com

FUATILIA SILSILA HII HUENDA ALLAH AKAJAALIA KHERI NDANI YAKE:

SEHEMU YA 1:
أعوذ بالله من الشيطان الرجيم
فلا أقسم بالشفق . والليل وما وسق. والقمر اذا التسق. لتركبن طبقا عن طبق.
      سورة الانشقاق :  ( 16-19 )
Katika aya zilotangulia hapo juu , ndani yake mna kiapo kutoka kwa allah sw, alie mmoja mlipaji wa viumbe kwa yale wanayoyatenda.
Anaapa allah sw, na (الشفق ) ash shafaq, yaani  mawingu mekundu,
Pia anawatangazia wanaotembea mchana katika harakati zao za maisha, na wale ambao wapo kwenye kuyaaga marhala haya ya maisha ya kidunia,  baada ya kua walikua watoto wadogo , kisha kuwafikia uzee, na hatimae kuondoka ulimwenguni.

Pia allah sw ameapa na usiku na kwa yale ambayo yamo ndani yake,
Ndani ya usiku kuna hali tofauti kwa waja ,  utawaona hawa wamo kwenye ibada wanasimama na kumsujudia  mola wao mlezi,  pia utawaona wengine wamo kwenye mambo yao ya kipuuzi,wakiwa wanashindana kumuasi allah sw,  pia utawaona hawa  wameghafilika    na wengine  wamelala,  halkadhalika ndivyo watu huwa wamelala  ila siku watakapokufa ndipo watakapoamka ,na watakapoamka haitowafaa wao kujuta kwao kwa kule kupoteza wakati wao bila kujivunia mema wala faida yoyote ile.
Tumuombe allah asitufanye kua miongoni mwao.

Pia allah sw, ameapa na mwezi pale unapokamilika ,  baada ya kua mwezi ulikua mchanga kabisa  kisha ukakua hali tofauti  mpaka ukafikia kukamilika kwa umbo lake kamili,
Vuta taswira hii na maisha yako wewe tangu unazaliwa mpaka kufikia ukubwa wako, jee  una mda gani ulobakisha wa kuishi katika dunia hii ?  

zinduka  hujacherewa !
Ikiwa hiyo ndio hali ilivyo  basi tambua ndugu muislamu   hakuna kwenye kukamilika kwa kwa kitu chochote ila huja mapungufu.
Tusiende sana usoni  ili kukupa fusra  wewe ndugu msomaji ili kuzingatia yaliyomo ndani ya maudhui hii.

TANB:
KUMBUKA KUA BORA YA MANENO NI YALE YALOKUA MACHACHE NA YAKALETA FAIDA.
Tuonane tena kwenye sehemu ya pili panapo majaaliwa ,

Ndugu yako katika imani   SULEIMAN OMAR SULEIMAN.   (ABDUL BARRY)
  KWA MAELEZO ZAIDI, NASAHA PIA USHAURI,  UNAWEZA KUTUMIA  ANUANI ILIYOPO HAPO JUU
                                                                                            والله أعلم
                                                                  والسلام عليكم ورحمة الله وبركاته

Comments