Safari ya kuelekea nyumba ya akhera
بسم الله الرحمن الرحيم.
الرحلة الى دار الآخرة
SAFARI YA KUELEKEA NYUMBA YA AKHERA
IMEANDIKWA NA :ABDULBARRY
Phone no: +255 778 682 699
+249 992 261 471
Email: suleimans003@gmail.com
FUATILIA SILSILA HII HUENDA ALLAH AKAJAALIA KHERI NDANI YAKE:
SEHEMU YA 2:
Ilipoishia sehemu ya kwanza:
Pia allah sw, ameapa na mwezi pale unapokamilika , baada ya kua mwezi ulikua mchanga kabisa kisha ukakua hali tofauti mpaka ukafikia kukamilika kwa umbo lake kamili,
Vuta taswira hii na maisha yako wewe tangu unazaliwa mpaka kufikia ukubwa wako, jee una mda gani ulobakisha wa kuishi katika dunia hii ?
zinduka hujacherewa !
Ikiwa hiyo ndio hali ilivyo basi tambua ndugu muislamu hakuna kwenye kukamilika kwa kwa kitu chochote ila huja mapungufu.
Endelea :
… baada ya kiapo hicho ambacho allah amekiapa ameweka jawabu la kiapo hicho mbele yake , na ni kama ifuatavyo:
" لتركبن طبقا عن طبق"
Maana yake ni kama ifuatavyo:
“ kwa hakika mtapanda (mtapitia) matabaka kwa matabaka”
Yaani, kwa yakini mtapitia kwa matabaka na madaraja mbali mbali, miongoni mwa mambo yenye kushuhudiwa hapa ulimwenguni,pia mtapitia mambo mengine yakiwa ya tabu na mifadhaiko nk.
Basi MAUTI ndio tabaka la mwanzo katika hayo, kwa maana ukiwa wajiandaa na safari hii hapa duniani basi tabaka la mbele yako ni mauti, na hakuna ujanja wa kuyakwepa basi jee! Vipi utayakabili?
Na marhala utazopitia ni kama ifuavyo :
MAUTI
MAISHA YA KABURINI
KUPULIZWA PARAPANDA LA KUFUFULIWA
KUKUSANYWA WAJA KATIKA UWANJA WA KUHESABIWA
IFUATIE KUPEWA KILA MMOJA DAFTARI LAKE
KUPIMWA MATENDO YA WAJA KWA MEZANI YA UADILIFU
KISHA WATU KUPITA KATIKA SIRAT
KILA MTU KULIPWA KWA ALIYOYAFANYA KATIKA MATENDO YAKE
NAAM,
Hii ndio hali ya safari yetu kwa mukhtasari, basi ni kwa kiasi gani ewe mja utaikabili safari hii,
Jee ni kwa hali gani utayakabili mauti?
Je ni zawadi gani utayoichukua ikufae kaburini?
Je hali itakuaje siku ya kufufuliwa?
Je hesabu yako umeiandaa kuwa upade gani?
Je utalipokea daftari lako kwa mkono gani?
Je mezani yako itakua nzito kwa amali gani?
Je utasalimika kuivuka sirati (daraja) ?
Je umeshajiandaa kukabidhiwa malipo yako?
Haya maswali yajaalie ni miongoni mwa mambo yako ambayo yanakupitikia akilini mwako kila siku,
Maswali hayo majawabu yake yapo kichwani mwako, siri yako wewe na nafsi yako, zinduka zingatia !
Na sehemu yetu ya pili itaishia hapa , usikose sehemu ya tatu kwa ufafanuzi wa marhala hizo kwa kadri allah atavyotuwezesha.
TANB:
KUMBUKA KUA BORA YA MANENO NI YALE YALOKUA MACHACHE NA YAKALETA FAIDA.
Tuonane tena kwenye sehemu ya tatu panapo majaaliwa ,
Ndugu yako katika imani SULEIMAN OMAR SULEIMAN. (ABDUL BARRY)
KWA MAELEZO ZAIDI, NASAHA PIA USHAURI, UNAWEZA KUTUMIA ANUANI ILIYOPO HAPO JUU
والله أعلم
والسلام عليكم ورحمة الله وبركاته
Comments
Post a Comment