Safari ya kuelekea nyumba ya akhera


بسم الله الرحمن الرحيم.
الرحلة الى دار الآخرة
SAFARI YA KUELEKEA NYUMBA YA AKHERA
IMEANDIKWA NA :ABDULBARRY
         Phone no: +255 778 682 699        
+249 992 261 471        
Email: suleimans003@gmail.com

FUATILIA SILSILA HII HUENDA ALLAH AKAJAALIA KHERI NDANI YAKE:

SEHEMU YA 3:
 Ilipoishia sehemu ya pili:
Jee ni kwa hali gani utayakabili mauti?
Je ni zawadi gani utayoichukua ikufae kaburini?
Je hali itakuaje siku ya kufufuliwa?
Je hesabu yako umeiandaa kuwa upade gani?
Je utalipokea daftari lako kwa mkono gani?
Je mezani yako itakua nzito kwa amali gani?
Je utasalimika kuivuka sirati  (daraja) ?
Je umeshajiandaa kukabidhiwa malipo yako?

Haya maswali yajaalie ni miongoni mwa mambo yako ambayo yanakupitikia akilini mwako kila siku,
Maswali hayo majawabu yake yapo kichwani mwako, siri yako wewe na nafsi yako,  zinduka zingatia !

Sasa endelea nayo …
    Katika sehemu hii ya tatu tutaleza marhala ambazo zilitangulia hapo  awali kama ilivyo katika sehemu ya pili , tunamuomba allah sw atuwafikishe kwa hilo.
Moja kwa moja tuanze na hii ambayo tuliitanguliza nayo ni kama ifuatavyo:
MAUTI
Elewa ewe ndugu kuwa mauti ni haki kwa kila mja, kama allah sw anavyoeleza kwenye kur ani,  (كل من عليها فان، )  kila kiliyomo ndani ya hii dunia basi ni chenye kumalizika (chenye kufa).

Mauti ni kitenganisho cha mawasiliano yako ya dunia na kukufanya uweze kuona mbali ambako hakuna mwenye kuweza kuona huko katika wanadamu ila kwa Yule ambaye taayari yupo kwenye safari hiyo au tayari mauti yameshamdiriki.

Elewa kuwa mauti ni kikato cha ladha ya dunia, hutenganisha baina ya mtu na swahiba yake hutenganisha baina ya mtu na kila alokuwa wa karibu yake.

Lakini istoshe hapo, tuweze kujua kua mauti ni kiywaji na kila mtu lazima anywe kinywaji hicho bila khiari .

Allah sw anasema :( قل يتوفىكم ملك الموت الذي وكل بكم... ) sema (ewe nabii kuwambia hao) atakufisheni malaika wa mauti ambaye amewakilishwa  kwenu (kwa kazi hii ya kutoa roho za viumbe)

Ewe mwanadamu hakika allah sw amemdhalilisha mwanadamu kwa mauti  na akaifanya dunia kuwa ndio nyumba ya kuishi tena yenye uhai wa kumalizika, maisha yenye kudanganya,  kama alivyoyaeleza hayo ndani ya qur an , )  وما الحياة الدنيا الا متاع الغرور ) hayakua haya maisha ya kidunia ila ni udanganyifu mtupu.

Wangapi yamewahadaa maisha hayo, je leo wako wapi?
Yuko wapi fir aun ?  yuko wapi hamana ?  yuko wapi qaruun?  Yuko abuu jahli ?  wako wapi kina Adi na thamudi?
Wako wapi pia waliomfano wa hao ambao nguvu, vyeo, utawala,nyadhifa mbalimbali  ziliwadanganya ?   hakuna shaka kuwa wapo kwenye adhabu mpaka siku ya kufufuliwa kwao.

Ikiwa dunia sio nyumba ya kudumu basi je ni kwa kiasi gani umeshajiandaa na maisha ya kudumu ambayo nimaisha ya  akhera ?

Hakika allah sw ametuleta hapa ulimwenguni kwa kututazama sisi waja wake ni yupi ambaye atafuata maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake,  kwani ameshabainisha hayo ndani ya kitabu chake

Allah sw anasema ( ...الذي خلق الموت والحياة ليبلوكم أيكم أحسن عملا...) allah ambaye ameyaumba mauti na akaumba uhai ili akujaribuni nyinyi waja  ni yupi kati yenu atakua na matendo mazuri zaidi…

NAAM, hakika allah sw ameyaumba mauti na uhai ili atujaribu ni yupi kati yetu amejipanga kwa ajili ya safari hii, tena kujiandaa kwa kiwango cha matendo mazuri zaidi, wala sio kiwango cha matendo mengi zaidi , kinachozingatiwa ni usahihi wa matendo hayo  jee yapo kama alivyoyafundisha allah sw kupitia mtume wake saw.

Au tumefanya matendo hayo kwa sababu nilimuona  babu akifanya, au Fulani kafanya namie nifanye,  elewa matendo sahihi ni yale yanayofanywa kwa mujibu wa mafundisho ya qur ani na muongozo wa mtume saw, kinyume na hapo amali hii itakua ni khasara kubwa siku ya kiama.

Tuishie hapa sehemu hii ya tatu, in sha allah  tutaendele na marhala hii sehemu ya nne panapo majaaliwa,  musinisahau kwa dua zenu njema , allah atupe ikhlas katika amali zetu.

Amiin.





Ndugu yako katika imani   SULEIMAN OMAR SULEIMAN.   (ABDUL BARRY)
  KWA MAELEZO ZAIDI, NASAHA PIA USHAURI,  UNAWEZA KUTUMIA  ANUANI ILIYOPO HAPO JUU
والله أعلم
والسلام عليكم ورحمة الله وبركاته

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUJIFUNDISHA QUR AN NA KUIFUNDISHA

SAFARI YA KUELEKEA NYUMBA YA AKHERA